Unataka kufanya kilimo biashara?

Pata ushauri wa kitaalam, pembejeo bora na vitabu vya kilimo bora vilivyosheheni mbinu za kisasa na miongozo sahihi itakayokuwezesha kuboresha kilimo chako na kuongeza mara dufu uzalishaji wa mazao yako.

Ushauri Kilimo

Kama unahangaika kutafuta mtaalam atakayekuongoza au kukushauri katika mradi wako wa kilimo, usihangaike tena, tupo kwa ajili yako.

Tunao wataalam wa kilimo watakaoshauriana na wewe kwa jambo lolote linalohusu kilimo biashara. Iwe ni suala dogo tu la kuzungumza kwa simu au jambo linalohitaji uchunguzi shambani au hata kuwa bwana shamba wako kwa kipindi chote cha uzalishaji wa mradi wako.

Wataalam wetu watakuwa bega kwa bega nawewe katika kila hatua ya utekelezaji wa mradi wako.

Unasubiri nini?

Bwanashamba-na-mkulima-wakishauriana-kwenye-shamba-la-maharage

Wataalam wazoefu

Utashauriwa na wataalam wabobezi katika kilimo, na sio watu tu. Wataalam wetu wana ujuzi na uzoefu wakutosha kwenye sekta ya kilimo. Hivyo, upo kwenye mikono salama.

Pembejeo bora

Tunazo pembejeo zilizothibitishwa na zenye ubora wa kuamika. Tutakupa mbegu bora za mazao, mbolea safi na viuatilifu vyenye ubora.

Weledi na Uadilifu

Weledi na Uadilifu ni nguzo muhimu katika utoaji wa huduma zetu. Tegemea kuhudumiwa kwa weledi na wakati wote huo amana yako itakuwa kwenye mikono salama.

Mwongozo-wa-kilimo-cha-nyanya

Vitabu vya Kilimo Biashara

Je, ungependa kuongeza ujuzi wako wa kilimo cha mazao mbalimbali?

Tuna vitabu vya kilimo bora na miongozo ya kilimo biashara. Vitabu hivi vina kila kitu unachohitaji kujifunza na kufanikiwa kwenye kilimo, kuanzia kuandaa shamba, kuchagua mbegu bora, kupanda, matunzo, mahitaji ya mbolea na viuatilifu hadi kuvuna. Bila kusahau, uchambuzi kamili wa gharama za uzalishaji katika kila hatua, pamoja na mapato tarajiwa baada ya mavuno.

Fanya maamuzi sahihi leo, kuwa mtaalam katika kilimo chako mwenyewe.

Shuhuda za wateja wetu

Miongozo yenu imenibariki sana!

Kwa kweli vitabu vinajieleza bayana sana kiasi kwamba hata mimi ambae sina uzoefu sana naweza tekeleza vyema miongozo ya vitabu. Nimeweza kujifunza njia bora za kilimo, awali sikujua kwanini napata mavuno hafifu lakini nimegundua ni kwa sababu sikuwa na elimu ya kilimo hasa kwenye kukabiliana na wadudu na magonjwa. Vitabu vya kilimo cha mahindi na nyanya vimenibariki sana.
Willy Mtae
Mkulima - Kinondoni, Dar

Vitabu vinaeleweka. Nimejifunza mengi!

Maelezo yanaeleweka, yametumia lugha rahisi kwa mkulima wa kawaida kuelewa. Niko naendelea kuvisoma na kutumia elimu nilioipata katika kilimo cha mazao niliopanda msimu huu. Nimegundua kuna baadhi ya hatua nilikuwa nakosea hivyo msimu ujao nitarekebisha hususani katika upandaji na uwekaji wa mbolea za kupandia.
Peter Shilogile
Daktari - Mbogwe, Geita

Punguzo la 17% kwa kila kitabu

Chagua kitabu chochote na upate punguzo la 17% sasa hivi. Bofya link hapa chini kupata offer hii …