About Us

Mogriculture TZ ni nini?
Mogriculture TZ ni kampuni inayojihusisha na uuzaji wa pembejeo za kilimo, utoaji wa elimu, mafunzo na ushauri wa kitaalam wa masuala ya kilimo kwa wakulima.
Tunatoa elimu na mafunzo ya kilimo kwa njia ya kuandika masomo ya kilimo na kuchapisha vitabu vya kilimo. Pia kwa magroup ya whatsapp. Unaweza kuona vitabu vyetu hapa.
Ushauri kilimo ni huduma tunayoitoa kwa moja kati ya njia hizi tatu: Online kwa simu, kutembelea mashamba na kuwa bwana shamba wako kwa msimu mzima. Karibu tushauriane leo.
Pembejeo tunazosambaza na kuuza ni pamoja na mbegu bora za mazao, mbolea, viuatilifu vya wadudu, magugu na magonjwa ya kuvu. Lakini pia, tunauza vifaa vya shambani kama vile pampu za kupulizia dawa, boot za shambani, n.k.
Mshauri kilimo: Mtalula
Naitwa Mohamed Mtalula.
Ni mtaalam wa kilimo mwenye shahada ya Sayansi ya Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo Morogoro, Tanzania.
Nilianzisha mtandao huu mwaka 2016. Nimekuwa kwenye sekta ya kilimo tangu nilipomaliza elimu ya juu, kama mtaalam wa kilimo Mtibwa Sugar Estates ltd ambako nipo mpaka sasa na ni mkulima kadhalika.
Pia ni Msimamizi Mwendeshaji na Mshauri wa masuala ya kilimo katika mtandao wa kilimo wa Mogriculture TZ. Ungependa kuchat nami? Bofya hapa.

